TUJIFUNZE
Habari za wakati huu mpenzi msomaji wa makala zangu. Nakuomba leo tuungane kidogo katika darasa hili la leo.
Ndugu msomaji leo naomba nikueleze kuwa "Ukifikilia kwa kina sana juu ya makosa yako utaweza kujifunza vitu vingi sana, ni mekaa nikafikilia nikaona kwamba wakati mzuri wa mtu kujifunza ni pale anapokosea. Siku .zote kosa linapaswa kutengeneza funzo akilini mwako na hii ni kwaajili ya kutokurudia tena"
Hakuna mtu yeyote mwenye kufanya zuri lolote pasipo kukosea, kulingana na hayo basi, kosa ni kiimalishi sha mazuri yetu. Makosa yako ya aina mbili na ambayo ni:
- Kukosea kwa kukusudia
- Kukosea kwa kutokukusudia
Kwa upande wangu kamwe sijisikii vibaya pale ninapofanya kitu ambacho ninajua kabisa niko sahihi ata kama wengi hawatapendezwa nacho,hii nikwasababu najiamini na nina hakika ya nifanyalo. Ukiwa katika safari nzima ya mafanikio jua kwamba watu wengi wanaangalia ni nini unafanya na wengi wao watakuwa wakipambana wakuangushe au usiweze kufikia sehemu unayoitaka wewe.
Dawa ya mtu anayekufuatilia ni kumfanyia vizuri ili nafsi imsute, ukiona mtu anakufuatilia sana jua hana kazi za kufanya sasa mpe kazi zako afanye na ambazo ni kufanya yako mengi apate cha kusimulia.
Kamwe usipende kubishana na watu kuhusu kitu ambacho unahakika ya kwamba hukufanya, maana utajichosha mno na utapoteza muda wako mwingi sana kwa vitu visivyokuwa na maana na kati ya vitu unavyopaswa kuviepuka ni kupoteza muda wako.