Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
11 Jun

KIOO

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #FANIKISHA MALENGO YAKO

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala zangu.

   Naomba leo tujifunze vitu vichache hivi lakini vyenye kuwa na maana kubwa katika maisha yetu ya kila siku.

  KIOO: Ndugu msomaji wa makala zangu najua utakuwa unajiuliza nikwanini leo nimekwandikia huu ujumbe lakini najuautajua baada ya kusoma mpaka mwisho. Kioo ni kifaa tukitumiacho kujitazama, je uliwahi kujiuliza kwamba kwanini unatumia Kioo nyumbani kwako?, kama uliwahi kujiuliza najua ulipata jibu kwamba tunajitazama kwenye Kioo ili tujirekebishe sehemu yenye dosari katika mwili wetu.

  Ndugu yangu kila mtu anasababu yake kuwapo na hivyo sasa sisi sote tunajifunza kila kitu kulingana na jamii inayotuzunguka. Kulingana na hayo sasa yatupasa kufanya yaliyo mema kwaajuili ya kuwafaidisha wale wajifunzao kutoka kwetu.

   Jiulize swali moja tu la kwamba kwanini mtu ajifunze kutoka kwako?, na hapo utaja ni namna gani uishi na ni nini ufanye ili kila anayefuata nyayo zako asipotee. Ndugu yangu nakuhasa kwamba kuwa mfano wa kuigwa ni utajiri tosha, jua ya kwamba kuwa tajiri sio mpaka umiliki majumba ya kifahari wala magari ya kifahari hapa ila utajiri ni vile vitu watu wanavyojifunza kutoka kwako.

KIOO
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974