Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
01 Jun

ACHA NIKUFUNGUE

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #FANIKISHA MALENGO YAKO

Habari za muda ndugu yangu?
Kama kawaida yangu naomba nikufungue kwa jambo hili ndugu yangu na msomaji mzuri sana wa makala zangu.
Kila zuri lazima liwe na mwanzo wake mgumu, usiogope kukutana vikwazo wala changamoto katika njia yako ya mafanikio. Malanyingi mtu akiwa anaanza kazi yoyote kwa mala ya kwanza iwe ni biashara au kazi ya kuajiliwa hukutana na mawazo yafuatayo baada ya kuanza.
Kwa upande wa anayeanza kufanya kazi kwenye ofisi ya mtu huwaza hivi, 'hivi mshahara huu unanitosha kweli?', 'hivi fulani analipwa shilingi ngapi', 'hivi nitapewa hela yangu kweli?', na mengine kama hayo. Siku zote kazi kazi zote ni ngumu kulingana na utendaji wako. Ukitaka kazi iwe ngumu itakuwa ngumutu ata ufanyeje, na mala nyingi vitu vinavofanya kazi kuwa ngumu huwa ni mawazo potofu kama hayo niliyoyataja hapo juu. Nikushauri kwamba unapopata kazi katika ofisi yoyote kwanza fanya yafuatayo;
-Ipende
-Ithamini
-Iiheshimu
-Ipe muda
-Jitume n.k
Kwa kufanya hayo utaona faida yake na hasara zake kwasababu utakuwa ushatimiza ni nini kazi yako inakupasa ufanye.
Siku zote mwanzo wa kazi huwa ni mgumu sana, na hii ni kwasababu unakuwa hujui mwelekeo wake lakini kwaa kufanya hayo niliyokweleza hapo juu kazi yako utaifurahia.

STARZTZ

ACHA NIKUFUNGUE
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974