FUNGUKA!!
Habari za muda huu mpenz msomaji wa makala zangu!! Natunaini hujambo kabisa.
Leo nakukaribisha tuweze kujifunza kwa pamoja au kuyajua machache niliyokwandalia siku ya leo.
SOMO: "Sioni sababu ya wewe kumweleza kila mtu shida zako, unajua ni kwanini? kwasababu hakuna zuri lijalo bila baya, hakuna mwenye kufanya yaliyosawa kila siku. Chamsingi kujua hapa ni kwamba unapokutana na hali ngumu au tatizo lolote katika safari nzima ya maisha, jifunza kutatua wewe mwenyewe kwanza kabla ya kuomba msaada kwa mtu mwingine.
Kama umeweza kutambua tatizo basi na kulitatua utaweza na hii ni sehemu ambayo unapaswa kuwa na moyo wa subira, ukakamavu, ujasili na mambo mengine kama hayo. Jua kwamba miongoni mwa marafiki zako, ni 26% tu inayopenda maendeleo na mafanikio yako. Jua ya kwamba hakuna rafiki yako anayefurahia pindi unapofanya kitu kizuri ukamzidi . Marafiki zako wa karibu watakuwa wa kwanza kukutolea maneno ya kejeli kwamba hutaweza na wewe sasa ndio wakati wako sasa kuonyesha ni kwa jinsi gani unaweza kuliko wao. Dawa ya adui yako ni kufanya mamb mazuri yatakayo mfanya azidi kujivuta zaidi kwako na kuzidi kuonekana jinsi gani alivo mnafiki.
Unapopata tatizo, jifunze kitu kupitia tatizo hilo na hyo itakuweka sehemu bora ya maendeleo yako.Kumbuka kila mtu alipitia mazingira magumu na anamengi ya kusimulia, hivyo basi mfundishe ulichojifunza baada ya wakati mgumu ulioupata na usimweleze magumu yaliyokupata.
TAMBUA THAMANI YAKO