Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
24 Aug

FANIKISHA MALENGO YAKO: Epsodi 1. Darasa letu la Fanikisha malengo yako linaanza leo...

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #FANIKISHA MALENGO YAKO

Jitahidi kufuatilia kila siku katika blog yangu ya STARZTZ, kwaajili ya kuelimika, kuburudanika, kuzijua habari na mengine mengi. Lakini pia napenda kukukaribisha kusoma kitabu changu hiki ambacho nitakuwa natoa elimu kila siku na ni kitabu chenye mwendelezo katika mada zifuatazo:
» KUJITAMBUA
»FANYA MAAMUZI SAHIHI
»MAHUSIANO
» BIASHARA
» UCHAGUZI WA MARAFIKI
» MALENGO MBADALABY
Elipidius g.mtagurwa


BY
Elipidius g.mtagurwa,
p.o.box70,
biharamulo
contact: +255 714260485 / +255 759 110974
Email: elipidiusgeofrey@gmail.com
Blog :www.chuyangcustarah.over-blog.com
Facebook: Chuyan’gCustarahEpsodi 1.
KUJITAMBUA
Ndugu msomaji, ninamaanisha nini nikisema neno kujitambua?
Watu wengi hushindwa kung’amua hili neno“Kujitambua” lakini mimi nimejalibu kukweleza kwa ufupi hapa chini.
“Kujitambua” ni ile hali ya mtu kujua yeye ni nani na anapaswa kufanya nini, wapi kwa wakati gani na kwa malengo gani.
Elimu hii ya kujitambua hupatikana kwa tabu sana kwani ni wachache wanaoelewa ni nini wanastahili kufanya. Kujitambua kunamfanya mtu kuonekana mwenye hekima katika uongeaji wake, Utii na huonekana kuwa na maarifa ya kuyajua mambo mengi ndani yake.

Kuna faida nyingi sana za mtu kujitambua
Moja wapo kuu ni hii ya kwamba mtu aliye jitambua, kila jambo alifanyalo linakuwa ni jambo la kuchochea maendeleo katika nafsi ya mtu na maendeleo ya jamii nzima inayomzunguka. Mara nyingi watu wa namna hii hutengwa na walio wengi na kupendwa na walio wachache, wakionekana kufanya vile kwasababu fulani kama wanaosema kupenda sifa, au kujiona na maneno mengine mengi ya kejeli. Walio wegi huyasema mengi yasiyona maana pasipokujua kwamba hiyo ndiyo njia sahihi ya kuiga.
Unapoamua kujitambua yakupasa kufanya au kuzingatia yafuatayo:
• Kuwa mtu jasili, Inamaana kuwa mtu wa kukubaliana na khali yoyote kulingana na mazingira uliyopo.
• Unapaswa kuwa mtu wa kutetea haki za wanyonge wanaooneekana sauti zao kutokusikika mbele za wengine.
• Kuwa mtu wa kutoa msaada wa aina yoyote unaohitajika kwa wakati na mahala husika.
• Usiwe mtu wa kukata tamaa kwa tatizo lolote ulionalo au kukutana nalo maana mengine hutokea kwa maana au mantiki fulani.
• Kuiga kila lililo jema na zuri ulionalo linaweza kuwa msaada kwako
• Usisite kumshauri na kumrudisha aliyeonekana kukata tamaa au kuvunjika moyo juu ya jambo fulani n.k.
Kupitia hayo na mengine kama hayo utaweza kueshimiwa na watu, utapendwa na utaonekana mtu tofauti sana na vijana wengine. Kwa ufupi utakuwa umeelewa ni nini maaana ya neno Kujitambua, na kama umeelewa ni vizuri ukamweleza mwenzio na ukamwonyesha kwamba wewe sasa umeelimika.

STARZTZ

FANIKISHA MALENGO YAKO: Epsodi 1.  Darasa letu la Fanikisha malengo yako linaanza leo...
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974