Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
01 Apr

HIZI NDIZO SHERIA 6 ZA CHINA AMBAZO KUNA UWEZEKANO KWAMBA ZILIKILETWA TANZANIA WATU WANAWEZA KUAMA NCHI...

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #HABARI

Tanzania ni moja kati ya nchi zenye amani na uhuru mkubwa kwa kuruhusu raia wake  kufanya vitu vingi lakini leo March 31 2017 naomba nikusogezee sheria sita za nchi ya Korea Kaskazini ambapo kama zikiletwa Tanzania itakuwa ngumu watu kuzitekeleza kutokana na utaratibu ambao tumezoea.

1: Style ya kunyoa nywele inachaguliwa na serikali

Hiki kinaweza kuwa ni kitu cha kushangaza sana lakini ni kweli  mwaka 2013 serikali ya Korea Kaskazini ilianzisha sheria ambayo inaipa mamlaka ya kuchagulia raia wake style Style za nywele 18 kwa wanawake na 10 kwa wanaume cha kushangaza zaidi style ya nywele ya Rais wa nchi hiyo Kim Jung Un haipo kwenye list iliyotolewa.

2: Serikali huchagua watu maalum wa kuishi ndani ya mji Mkuu.

Korea Kaskazini watu maalum waliochaguliwa na serikali ndio wanaruhusiwa kusihi ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo, kosa kisheria kwa mtu kuingia mjini  Pyongyang bila kibali maalum cha kuingia katika mji huo.Watu wenye mafanikio na wenye utii kwa serikali ndo huruhusiwa kuishi katika mji huo.

3: Ni lazima watu kupiga kura.

Kwa kawaida kupiga kura ni jambo la hiari nchi zote duniani lakini ukiwa Korea Kaskazini ni lazima upige kura, nchi hiyo hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano lakini cha kushangaza hakuna mgombea aliyewahi kujitokeza kushindana na Kim kwenye uchaguzi mkuu.

4: Ni lazima kuangalia TV ya Taifa.

Wananchi wa Korea Kaskazini huruhusiwa kuangalia channel tatu pekee ni kosa la kisheria kuangalia program za Tv kutoka nchi zingine hasa Marekani na ni lazima wananchi kuangalia Televisheni ya Taifa kujua kinachoendelea nchini mwako.

5: Wananchi hawaruhusiwi kumiliki bibilia.

Ukiwa Korea Kaskazini ni kosa kisheria kumiliki bible au kuamini katika ukristo, serikali ya nchi hiyo inaamini kwamba ukristo ni dini ya nchi za magharibi hivyo serikali ndio taasisi ya inayotakiwa kuabudiwa na wananchi wa nchi hiyo.

6: Ukitoroka jela wanaoadhibiwa ni familia yako.

Ukitoroka jela Korea Kaskazini wanaoadhibiwa ni familia yako mpaka kizazi cha tatu yaani kuanzia wewe,watoto utakaowazaa na wajukuu zako, sheria hii iliwekwa ili kuzuia watu kutoroka jela  licha ya kuwa ilipingwa vikali na umoja wa kimataifa (UN).

HIZI NDIZO SHERIA 6 ZA CHINA AMBAZO KUNA UWEZEKANO KWAMBA ZILIKILETWA TANZANIA WATU WANAWEZA KUAMA NCHI...
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974