Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
03 Apr

ARSENAL WAKUBALI KUTOKA SALE YA BAO 2-2 DHIDI YA MANCHESTER CITY, ANGALIA HAPA CHINI...

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MICHEZO

Jumapili ya April 2 2017 game za Ligi Kuu England zilichezwa kama kawaida ila game ya Arsenal dhidi ya Man City ndio  ilikuwa game inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa EPL, Arsenal walikuwa wenyeji wa Man City katika uwanja wa Emirates. Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamejikuta wakiambulia sare ya kufungana goli 2-2, magoli ya Arsenal yakifungwa na Theo Walcott dakika ya 40 baada ya Leroy Sane kuifungia Man City goli la kuongoza dakika ya 5 na Sergio Aguero akapachika goli la pili ambalo lilisawazishwa na  Shkodran Mustafi dakika ya 54. Sare ya Arsenal dhidi ya Man City inakuwa ni sare yao ya 45 toka wakutane November 11 1893 katika mchezo uliyomalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa goli 1-0 ila Man City ilikuwa ikiitwa Ardwick wakati huo, wamekutana mara 190, Man City akishinda mara 50 na Arsenal akishinda mara 95.

ARSENAL WAKUBALI KUTOKA SALE YA BAO 2-2 DHIDI YA MANCHESTER CITY, ANGALIA HAPA CHINI...
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974