Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
15 Mar

VIDEO: PAUL MAKONDA AJA KWA KASI AKISEMA YEYE SIYO MWANASIASA ANAYETAFUTA SIFA ZA KIJING!!!....

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MATUKIO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo March 14 2017 ametembele moja kati ya maeneo yaliyokubwa na Mafuriko yaliyotokana na mvua iliyotokea March 13 2017, Buruguni  Mnyamani ndipo Paul Makonda ametembea na ameagiza   Nyumba 36 zilizokuwa pembezoni mwa Bonde la Mto Msimbazi kuanza kuvunjwa kesho.

Kuna Nyumba 36 zitaanza kubomolewa kesho na Nyumba hizo zimegawanyika kwenye makundi matatu kundi la kwanza wameshalipwa na wameshapewa viwanja Mabwepande la pili kuna watu pia wamepewa Mwabwepanda wamejenga kule na huku wamepangisha na kundi la mwisho ni wale ambao hawajapata fidia zao’- Paul Makonda

Wale ambao wamejenga pembezoni mwa Mto au umejenga pembezoni kwenye mabonde ni waambie ukweli hakuna pesa yeyote ambayo watapata ngoja niseme tu ukweli mimi si mwanasiasa ninayetafuta sifa za kijinga acha niwaambie tu ukweli‘-Paul Makonda, Nimekusogezea Video yake hapa chini.

VIDEO: PAUL MAKONDA AJA KWA KASI AKISEMA YEYE SIYO MWANASIASA ANAYETAFUTA SIFA ZA KIJING!!!....
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974