LORI LABIRINGITA MWELEKA WA NGUVU BAADA YA KUACHA NJIA NA KUANZA KUCHANJA MBUGA HUKO WILAYANI MAKETE
Lori aina ya Isuzu TX lenye namba za usajili T 721 BVV lililokuwa limebeba mawe likiwa limepinduka katika kijiji cha Masisiwe na kusababisha majeruhi na kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa katika lori hiloTaarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa lori hilo lilipoteza muelekeo ghafla kisha likaanza kupinduka kwa kubiringika mara kadhaa umbali unaokadiriwa kuwa zaidi ya mita 80 kutoka barabarani