Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
16 Mar

HARMORAPA AAMBULIA BURUNGUTU LA MATUSI BAADA YA KUNUNUA KESI YA DIAMOND NA ALIKIBA...

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #VIJIMAMBO

Dogo Harmorapa ainunua bifu ya Diamond na Alikiba, achezea mvua ya matusiHarmorapa ni kama amemwaga petrol kwenye moto wa gesi. Rapper huyo aliyeteka vichwa vya habari kwa sasa nchini ameonekana kuanza kuununua ugomvi wa Diamond na Alikiba.Harmo kupitia mtandao wa Instagram, amemtuhumu Diamond kuwa ndio aliyeanza kumchokoza Kiba hivyo anapaswa kumuomba msamaha kupitia vyombo vya habari. Kupitia mtandao huo hitmaker huyo wa Kiboko ya Mabishoo ameandika:
Mimi harmorapa mfalme wa bongoflaver and social network kwa sasa nasema kiukweli kutoka moyoni bwana mdogo #diamondplatnumz wewe ndo ulie anza kumrushia vijembe vya dharau Fundi #alikiba sasa usitafute suluhu kirahisi rahisi wewe platnumz nenda kwenye midia piga goti Muombe msamaa Alikiba kwani mkosefu ni wewe na sio Alikiba .
akammalizia kwa kusema Now naitwa Harmo Rapa simba

Matokeo ya alichokiandika si mazuri. Hadi tunaenda mtamboni, bado anachezea mvua ya matusi kutoka kwa Team Diamond.

STARZTZ

HARMORAPA AAMBULIA BURUNGUTU LA MATUSI BAADA YA KUNUNUA KESI YA DIAMOND NA ALIKIBA...
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974