Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
01 Dec

HII NDIYO ADHABU ALIYOIPATA KOCHA WA MANCHESTER UNITED BAADA YA KOSA LA UTOVU WA NIDHAMU...

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MICHEZO NA BURUDANI

November 30 2016 katika habari zilizoshika headlines zetu ni pamoja na hii kuhusiana na kocha wa Man United Jose Mourinho ambapo chama cha soka England FA kimetangaza kumfungia mechi moja kukaa katika benchi na kumpiga faini ya pound 16,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 40 kwa utovu wa nidhamu.

Mourinho amepewa adhabu hiyo kutokana na kosa la kupiga chupa ya maji kwa hasira wakati wa mchezo wa Man United dhidi ya West Ham United uliomalizika kwa sare ya goli 1-1, Mourinho alipiga chupa hiyo baada ya refa Jon Moss kumuonesha kadi ya njano Paul Pogba kwa kujianguasha.

screen-shot-2016-11-30-at-8-54-55-pm

Kama utakuwa unakumbuka Jose Mourinho hilo litakuwa kosa la pili kulifanya ndani ya mwezi mmoja, baada ya October 29 kutolewa katika benchi katika mchezo dhidi ya Burnley na baadae  FA ikampiga faini ya pound 8,000 na kufungiwa mechi moja kukaa katika benchi.

HII NDIYO ADHABU ALIYOIPATA KOCHA WA MANCHESTER UNITED BAADA YA KOSA LA UTOVU WA NIDHAMU...
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974