WILAYANI BIHARAMULO, WATU WALIA NJAA KWASABABU YA UPATIKANAJI DUNI WA CHAKULA, WADAI JUA NDO CHANZO...
Ndugu msomaji wa Makala zangu leo nikiwa katika Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera nimekutana na wakazi mbali mbali katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hii na kusikiliza kero zao kuhusiana na suala zima la uoatikanaji wa chakula. Nikiwa katika kijiji cha Nyakatuntu nimekutana na mzee mmoja (mzawa mkongwe) akijalibu kunielezea hali halisi ya uhaba wa chakula kwa kipindi hiki. Mzee huyo amesema Msimu huu wameshindwa kupanda Mazao mengi sana sana Mahindi na Maharagwe kwasababu ya Kukosa Mvua.
Ameendelea akisema Mvua imesababisha ata kukosekana kwa Ndizi Na ikiwa Ndizi Ndilo zao wanalolitegemea kwa kiasi kikubwa.