Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
04 Nov

VIDEO:MISS KILIMANJARO, GRORY MINJA KUTOKA KATIKA TOP 10 YA KUMSAKA MISS TANZANIA ASAINI MKATABA WA KAMPUNI YA MAGA "PII"...

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MATUKIO

Ni siku chache sasa toka mashindano ya kumsaka miss Tanzania 2016 kumalizika hivi karibuni ambapo Fainali zake zilifanyika kwenye jiji la Mwanza kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo miaka zaidi ya ishirini iliyopita, Miss Tanzania 2016, Diana Lukumai aliitangazwa mshindi wa taji hilo.

Licha ya kutokuwa mmoja ya washiriki walioingia top ten, mrembo ambaye ni Miss Kilimanjaro, Glory Minja Leo November 3 2016 amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja kuwa balozi wa Kampuni ya Teknolojia ya Magari ‘PII’.

Akizungumza kuhusu mkataba huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Teknolojia ya Magari ‘PII’, Ebenezer Msuya amesema kampuni yao imeingia mkataba na Glory kutokana na uwezo ambao ameonyesha kwa kipindi ambacho walikuwa wakidhamini mashindano ya Miss Tanzania na baada ya kutambua uwezo wa washiriki hao walibaini kuwa Glory ana uwezo wa kufanya nao kazi.

>>>’Tumesaini naye mkataba wa kufanya kazi, leo tumemkabidhi cheque ya milioni lakini vilevile tumesaini naye mkataba wa mwaka mmoja ambao tutakuwa tunafanya nae shughuli za kijamii pamoja na shughuli nyingine za kimasoko’;- Msuya.

kulikuwa na vigezo walikuwa wanavihitaji mimi binafsi kuna vitu nilivifanya, walitupatia business card kwa kuwa walijua tutazunguka mikoa

Kwa upande wa Miss Kilimanjaro 2016 ambaye pia ni mshiriki wa Miss Tanzania, Glory Minja amesema ni nafasi ya kipekee kufanya kazi na kampuni hiyo ambayo imejikita zaidi katika teknolojia na atatumia nafasi aliyonayo katika jamii kuhakikisha anafanikisha malengo ambayo wanataka kuyafikia.

VIDEO:MISS KILIMANJARO, GRORY MINJA KUTOKA KATIKA TOP 10 YA KUMSAKA MISS TANZANIA ASAINI MKATABA WA KAMPUNI YA MAGA "PII"...
VIDEO:MISS KILIMANJARO, GRORY MINJA KUTOKA KATIKA TOP 10 YA KUMSAKA MISS TANZANIA ASAINI MKATABA WA KAMPUNI YA MAGA "PII"...
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974