Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
10 Nov

RAIS MAGUFULI AONYESHA UZALENDO BAADA YA MKE WAKE MAMA JANETH KUUGUA NA KUMLAZA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI...

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #HABARI

LIMEKUWA jambo la kawaida kwa viongozi  mbalimbali na familia zao kutibiwa nje ya nchi au katika hospitali zinazotambulika kama za watu wenye hadhi na fedha lakini suala hili limekuwa tofauti kabisa kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli.
Rais Magufuli amedhihirish uungwana uzalendo wake kwa kitendo cha mke wake kutibiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 

 

Rais Magufuli ameonekana Hospitalini hapo leo  akielekea wodini kujulia hali mkewe mama Janneth Magufuli.
suala hili limeonyesha kuwa Rais anawapenda wananchi wake kama anavyopenda nafsi yake ambapo mkewe amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo ambayo huwahudumia wananchi wote.

 

jambo ambalo limetofautiana viongozi wengi ambao hukimbilia kwenye hospitali za nje ya nchi
suala hili litazidi kuwapa imani wananchi kwa Rais wao kutokana na kuamini anachosimamia.Amepigania Hospitali ya Muhimbili kuwa hopitali itakayotoa huduma nzuri kwa wananchi wote.
Amepigania kuboresha mazingira ya matibabu katika hospitali hiyo. na hospitali nyengine nchini. 
 
Kama kawaida ya Rais Magufuli haikutosha kumona mkwe tu. aliwajulia hali na wagonjwa wengine.
RAIS MAGUFULI AONYESHA UZALENDO BAADA YA MKE WAKE MAMA JANETH KUUGUA NA KUMLAZA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI...
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974