Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
24 Oct

MANCHESTER UNITED WAKUBALI KULALA KWA KIPIGO CHA BAO 4-0 KUTOKA KWA CHERSEA....

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MICHEZO

Ikiwa ni jumapili ya October 23 2016 ndio siku ambayo kocha wa Man United Jose Mourinho alirudi tena Stamford Bridge kwa mara nyingine kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ya Chelsea akiwa kakaa upande wa timu za wageni, Mourinho safari hii alirudi Stamford Bridge akiwa kocha mkuu wa Man United baada ya kufukuzwa na Chelsea December 17 2015.

39a32a2e00000578-3864700-image-a-1_1477239572184

Kwa bahati mbaya licha ya Jose Mourinho kuwa na heshima kubwa katika klabu hiyo alikaribishwa kwa kushuhudia Man United ikifungwa kwa mara ya 51 na Chelsea, licha ya kuwa Man United ni wababe kwa rekodi kwa kuwahi kuwafunga Chelsea kwa mara 75, huku wakiwa wamesuluhu mara 49, wamekubali kipigo cha goli 4-0.

39a35be700000578-3864700-image-a-55_1477241423069

Kikosi cha Chelsea kilichokuwa chini ya kocha muitaliano Antonio Conte kiliiadhibu Man United kwa kuifunga goli 4-0 licha ya kuwa Man United waliutawala mchezo kwa asilmia 56 kwa 44, magoli ya Chelsea yalifungwa na Pedro Rodriguez dakika ya 1, Garry Cahill dakika ya 21, kipindi cha pili dakika ya 62 Eden Hazard akaua dalili za Man United kutafuta walau suluhu.

39a36c6d00000578-3864700-image-a-59_1477241519530

Goli la Ngolo Kante dakika ya 70 ndio lilifanya mashabiki wa Man United waanze kuondoka uwanjani wakiwa hawana matumaini tena ya kupata matokeo katika mchezo huo, Man United sasa anakuwa kafungwa mchezo wa  tatu wa EPL msimu huu katika mechi zake tisa alizocheza za Ligi Kuu England.

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974