VIDEO: RAIS WA TANZANIA MHE MAGUFULI AZINDUA NDEGE MPYA ZA TANZANIA...
Ni leo September 28, 2016 Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua Ndege mpya mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kwaajili ya kutumiwa na kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Uzinduzi huu umefanyika katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu julius Nyerere jiijini Dar es Salaam. Rais Magufuli amezungumzia uwezo wa Ndege hizo kwa wanaozibeza Ndege hizo.>>>"Ukitumia Ndege ya Jet kutoka hapa mpaka Songea utatumia milioni 28.9 za Mafuta, ukitumia NDege hii ni milioni moja kwahiyo kwa watu wanaofanya biashara lazima waipige vita na utofauti wa kufika ni dakika 20, dakika 20 ukichelewa wewe zinakuuma nini na ndio maana yule aliyezungumza anataka speed akapande za Jeshi."