ATUPWA JERA MIAKA 30 KWA KULAWITI MSICHANA MAKABURINI...
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemhukumu Ally Rashidi maarufu kwa jina la Ally mwizi kifungo cha miaka 30 Jela baada ya kupatikana na hati ya kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 25 Makabulini, hukumu hiyo iliyovuta hisia za watu wengi na manispaa ya Mpanda ilitolewa jana na Hakimu wa wa Mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka pasipo kutia shaka, ukiongozwa na mwanasheria wa mkoa wa Katavi, Jamila Mziray.