Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
02 Jun

Mlundwa afungiwa miaka 5

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MICHEZO NA BURUDANI

Mlundwa afungiwa miaka 5

SERIKALI imemfungia kwa miaka mitano Rais wa Shirikisho la Ngumi (PST), Emmanuel Mlundwa na taasisi yake kujihusisha na masuala ya kuratibu ngumi za kulipwa ndani na nje ya Tanzania kuanzia jana Mei 31 hadi Mei 31 mwaka 2020.

Imefikia hatua hiyo ya baada ya PST kuratibu pambano kati ya Thomas Mashali na Sadjadi Meherab wa Iran jijini Dar es Salaam Mei 14, mwaka huu ambapo pia PST ilichezesha watoto wenye umri wa miaka 10.

Aidha, PST imeadhibiwa kwa kumwajiri mtoto mwenye umri wa miaka minane (jina tunalo) aliyetumika kutangaza raundi za mchezo huo.

“Juni 18, 2002 tuliwaandikia PST barua yenye kumbukumbu namba KVJM/MK/SR/1/28/87 iliyowataka PST kutoa maelezo ya kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kosa la kuidhalilisha serikali juu ya uridhishwaji wake wa mikataba ya nje yenye kupinga ajira kwa watoto, na kazi ngumu kwa watoto,” alisema Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),” Mohammed Kiganja.

“Serikali inaamini mchezo wa ngumi una utaratibu wake na taratibu zake zote ni ngumu kwa watoto chini ya miaka 18 kupambanishwa, ngumi za kulipwa mashindano ya vijana ya dunia huanza kupambanishwa wakiwa na umri wa miaka 21 hadi 23 na ngumi za ridhaa ndio waliopewa jukumu la kuibua, kukuza na kuviendeleza vipaji, vijana kucheza kwa taratibu zenye kuwalinda na kuzingatia afya na maadili ya mabondia hao nchini,” alisema.

Kiganja alisema baada ya kupitia utetezi wa barua yake Mei 26 hautofautiani na majibu aliyomjibu katibu mkuu mwaka 2002, ambapo alimnukuu na kusema “ PST ipo tayari kupokea na kutekeleza maagizo ya kusitisha mapambano ya watoto, ikiwa ni maoni kuwa kusitisha huko kutazorotesha maendeleo ya mchezo huo kwa maana watoto hao ndio wanategemewa kuunda timu ya tiafa kwa mashindano mbalimbali ya kidunia.”

Alisema BMT ilitegemea majibu ya Mlundwa ambaye ni bondia wa zamani uzito mwepesi aliyeweka historia ya kuliletea heshima taifa kupitia mashindano ya Olimpiki, Jumuiya ya Madola na Michezo ya Afrika katika medani ya ngumi za ridhaa, amekuwa mstari wa mbele kuzishawishi Kenya na Uganda kuanzisha vyama vya ngumi za kulipwa, yangelenga kueleza mamlaka iliyomridhia kuandaa ngumi za watoto nchini Tanzania lakini hakufanya hivyo.

“Maelezo yake mengi na picha hazionyeshi kama ana kibali cha nchini cha kuvunja mikataba iliyoridhiwa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO), yenye kupiga vita ajira ya watoto na kazi ngumu na mbaya zinazoweza kumuathiri mtoto kwa ujumla wake. “Kwa kuwa kitendo hichi ni mara ya pili serikali inaona ameidharau, ameidhalilisha kimataifa kwa kutoa ajira kwa watoto mfano kumwajiri mtoto mwenye miaka nane, hiyo ni kuipuuza serikali, PST kazi yake kubwa ni biashara ya ngumi za kulipwa hakuna hata katiba, kanuni inayoikasimia PST kufanya kazi ya maendeleo ya ngumi nchini’’, alisema.

Mlundwa amekuwa kiongozi wa ngumi tangu mwaka 1980 alipoanzisha chama cha BUT baadaye kikabadilishwa jina na kuwa TPBC alichodumu nacho kwa miaka saba, kabla ya kwenda masomoni nje ya nchi na kukiacha chama mikononi mwa Bakari Suleiman na baadaye kupitia mikononi mwa Emmanuel Saleh, Onesmo Ngowi na Chaurembo Palasa.

STARZTZ

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974