Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
30 May

SERIKALI KUFUFUA MASHAMBA YOTE YA KILIMO NA MIFUGO.

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #HABARI

SERIKALI KUFUFUA MASHAMBA YOTE YA KILIMO NA MIFUGO.

SERIKALI imeamua kufufua mashamba yote ya kilimo na mifugo nchini.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba amesema kwa kuanzia, wiki ijayo maofisa wa Benki ya Kilimo Tanzania watatembelea shamba la mifugo la Kitulo, Makete.

Hatua hiyo inatokana baada ya kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Daud Yassin aliyekumbushia ahadi ya kufufua shamba hilo.

Mwigulu alisema hayo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko (CCM) aliyehoji sababu za kituo cha kuzalisha mbegu cha Bugaga kutelekezwa.

Kwa mujibu wa Mwigulu, serikali itafufua mashamba yote na imekuwa katika maandalizi tofauti kuhakikisha mashamba hayo yanafufuka.

“Nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa mashamba yote ya mifugo na kilimo yanafufuka. Tunafanya maandalizi kwa kila eneo husika. Tutahakikisha tunafanya utaratibu wa kuyafufua ili kusaidia vijana katika kilimo na masoko,” alieleza Mwigulu.

Katika majibu yake kuhusu shamba la mbegu la Bugaga, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alisema limekaa kwa muda mrefu bila ya kuzalisha kutokana na ufinyu wa fedha, limepangwa kufufuliwa katika mwaka 2016/17 lizalishe mbegu kwa wingi.

Hivi karibuni, Waziri Mwigulu alikutana na Mkuu wa Wilaya ya Makete aliyefika mjini hapa kuonana naye ili kukumbushia ahadi yake ya Machi mwaka huu alipotembelea shamba la Kitulo na kuahidi serikali italifufua shamba hilo.

STARZTZ

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974