Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
16 May

RASHFORD ATAJWA KIKOSI CHA UINGELEZA CHA EURO.

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MICHEZO

RASHFORD ATAJWA KIKOSI CHA UINGELEZA CHA EURO.

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amemtaja chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford kwenye kikosi chake cha wachezaji watakaocheza Euro 2016.

Rashford, 18, alianza kuchezea timu kuu ya Uinted kipindi cha pili cha msimu lakini aliwika mara moja.

Alifunga mabao manne mechi zake mbili za kwanza na aliwafungia mabao saba katika mechi 16 tangu aanze kuwachezea 25 Februari.

Hodgson ametaja kikosi cha wachezaji 26, ambacho kitapunguzwa baadaye hadi wachezaji 23.

Winga wa Newcastle United Andros Townsend na kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere pia wamo kwenye kikosi hicho kitakachopigania ubingwa Ufaransa, kwenye michuano hiyo itakayoanza tarehe 10 Juni.

STARZTZ

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974