Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
04 May

MMILIKI WA JUMBA LILILOPOROMOKA AACHILIWA KENYA.

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #HABARI

MMILIKI WA JUMBA LILILOPOROMOKA AACHILIWA KENYA.

Mmiliki wa jengo lililoporomoka mjini Nairobi ,Kenya na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana ya dola 5000 kila mmoja wao.

Walikana mashtaka ya kuua bila kukusudia.

Hakimu alisema kuwa hakuna sababu mwafaka ya kuwazuilia washukiwa.

Upande wa mashtaka ulitaka kuwazuia kwa siku 21 ili kupata muda wa kumaliza uchunguzi wao.

Jumba hilo la ghorofa sita lilianguka kufuatia mvua kubwa na kuwaua takriban watu 26 huku maafisa wa serikali wakisema kuwa watu 90 wengine hawajulikani waliko.

Mamlaka ya jiji la Nairobi imesema kuwa jumba hilo lilikuwa limepangiwa kuvunjwa baada ya kubainika kwamba sio salama kwa watu kuishi.

STARZTZ

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974