Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
21 Apr

TUNDA MAN AZUNGUMZIA AJALI ALIYOIPATA

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #MICHEZO NA BURUDANI

Mkali wa Ngoma ya Mama Kijacho, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ amezungumzia ajali aliyopata hivi karibuni katikati ya Idetelo na Makambako na kusababisha kifo cha mshkaji aliyekuwa naye, Kapizo kuwa, amejifunza mengi ikiwemo suala la kumuabudu Mungu linapaswa kuwa wakati wote.
Akizungumza nasi Tunda Man alisema hiyo ni ajali kubwa kwake kukumbana nayo na inatakiwa kumtanguliza Mungu mbele kwa maana hakuna binadamu anayefahamu juu ya kifo chake kitamkuta lini, wapi na akiwa anafanya kitu gani.
“Kapizo tumempumzisha Jumatatu hii kwao huko Kilosa lakini kiukweli nimejifunza mambo mengi kutokana na ajali hiyo, zaidi ninamshukuru Mungu kunibakiza hai, sikupata majeraha sana japo ajali ilikuwa kubwa,” alisema Tunda Man.

STARZTZ

TUNDA MAN AZUNGUMZIA AJALI ALIYOIPATA
Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974