RAIS OBAMA APINGA MATUMIZI YA NGUVU ZA NNJE SULUHU YA MGOGORO WA SYRIA...
Rais Obama amesema kuwa, itakuwa ni makosa makubwa kwa mataifa ya Magharibi kutuma majeshi yake hadi Nchini Syria ili kumuondoa madarakani Rais wa Syria Bashar al-Assad.Akizungumza na BBC, Obama amesema si busara hata kidogo kuwatuma wanajeshi wa Nchi kavu nchini Syria kumpindua Rais assad kwasababu hilo pekee halitasuluhisha matatizo ya Syria.