Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
23 Apr

RAIS MAGUFULI AIOMBA CANADA KISHIRIKIANA KATIKA KUKUZA UCHUMI

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #HABARI

RAIS MAGUFULI AIOMBA CANADA KISHIRIKIANA KATIKA KUKUZA UCHUMI

Rais JOHN MAGUFULI ameiomba CANADA kushirikiana na TANZANIA katika kuleta mageuzi ya kiuchumi, hususani katika uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo, Madini, Uvuvi na Huduma za kijamii ametoa kauli hiyo Jijini DSM wakati akizungumza na Balozi wa CANADA nchini ALEXANDRE LE'VE'QUE aliyekutana nae Ikulu Jijini DSM na kupokea barua yenye ujumbe wa Waziri Mkuu wa CANADA, JUSTIN TRUDEAU.
Rais MAGUFULI amesema kuwa TANZANIA hairidhishwi na jinsi kilimo kisivyowanufaisha wakulima hapa nchini na kuitaka CANADA kushirikiana na TANZANIA kujenga viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na uvuvi ili kuzalisha ajira na kuongeza thamani ya mazao.
Kwa upande wake Balozi LE'VE'QUE amemhakikishia Rais MAGUFULI kuwa atafikisha ujumbe huo kwa Waziri Mkuu CANADA, -TRUDEAU na amebainisha kuwa nchi hiyo ipo tayari kushirikiana na TANZANIA katika juhudi zake za kuimarisha uchumi.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amepokea ujumbe kutoka kwa Rais wa ALJERIA, ABDELAZIZ BOUTEFLIKA ambaye amepongeza hatua anazochukua katika uendeshaji wa serikali, amemhakikishia kuwa ALJERIA ipo tayari kuendeleza na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo.
Ujumbe wa Rais Bouteflika umewasilishwa kwa Rais na Balozi wa nchi hiyo hapa nchini BELABED SAADA.
Katika hatua nyingine, Rais MAGUFULI ameagana na Balozi wa VATICAN, FRANCISCO MONTECILLO ambaye anamaliza muda wake baada ya kuiwakilisha VATICAN kwa muda wa miaka minne na nusu.

STARZTZ

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974