Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
25 Apr

MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #VIJIMAMBO

MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU
MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMUMADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU

Kwa miaka mingi sasa, baadhi ya watu wamegubikwa na dhana potofu ya kwamba, kuwa mweupe ndiyo urembo.

Dhana hii imewafanya wengi waanze kutumia vipodozi vikali, bila kujali madhara ya baadaye.
Kwa mfano, hata baadhi ya wasanii, wake kwa waume, wamekuwa wakijibadili ngozi zao na tumewaona wakibadilika hatua kwa hatua.

Hata hivyo, unapohisi kuna uzuri, mara nyingi kuna kudhurika. Madhara ya awali ya vipodozi hivi, huonekana kwa mtumiaji kubabuka ngozi, kuwa na mabaka meusi au ngozi kuwa nyekundu. Lakini yapo madhara mengine mabaya zaidi ya hayo.

Katika bidhaa hizo zinazotumika za kujichubua, kuna kemikali za aina mbili.
Kwanza ni ‘Hydroquinone’ na ya pili ni ‘Mercury’.
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira.
Hutumika pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele.

MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU

1. BITHIONOL
Kupata mzio wa ngozi/allergic na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua.

2. HEXACHLOROPHENE
• Inapenya kwenye ngozi na kuingia kwenye ishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu hasa kichwani.
• Pia inasababisha ugonjwa wa ngozi na kuathirika kwa ngozi pindi unapokuwa kwenye mwanga wa jua.
• Kwa watoto wachanga husababisha uhalibifu kwenye ubongo
• Vile vile ngozi inakuwa laini na kusababisha kupata ugonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi.

3. ZEBAKI (MERCURY)
• Husababisha madhara ya ngozi, ubongo, figo na viungo, mbalimbali vya mwili
• Zebaki inapopakwa kwenye ngozi kuweza kupenya taratibu ndani ya mwili na kusababisha sumu yake kuingia kwenye damu na kusababisha madhara mwengi mwilini.
• Mama mjamzito akitumia vipodozi vyenye zebaki mtoto huathirika akiwa akiwa bado tumboni na huzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.
• Husababisha ngozi kwa laini na kuwa na mabaka meusi na meupe
• Husababisha mzio/ allergic wa ngozi na muwasho
• Sumu iingiapo kwenye mishipa ya fahamu husababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu.
• Sumu ya zebaki ikiingia mwilini kwa kiwango kikubwa husababisha madhara maka upofu, uziwi, upotevu wa fahamu wa madhara mara kwa mara.

4. VINYI CHLORIDE
• Inasababisha kansa ya maini, ubongo, mapafu na mfumo wa damu
• Sumu pia husababisha kuumwa kichwa, ksikia kizunguzungu na kupoteza fahamu

5. ZIRCONIUM
Husababisha kansa ya mapafu na ngozi

6. HALOGENATED SALICYLANILIDE
• Husababisha mzio wa ngozi mara inapopata mwanga wa jua
• Husababisha ugonjwa wa ngozi

7. CHLOROQUINONE
• Kundi zima la vipodozi vya CHLOROQUINONE hutumika kutengenezea vipodozi lakini kiambato ambacho kinachotumika ziaid ni kiambato cha Hydroquinone.

8. HYDROQUINONE
• Husababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, kansa, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meusi na meupe.

9. STEROIDS
• Steroids ni kundi la homoni, homoni hizi hutenganezwa kwenye miili ya binadamy na wanyama. Pia zinaweza kutengenezwa nje ya mwili wa binadamu yaani bandia (artificial). Katika kundi hili, corticosteroids ndizo hutumika sana kama viambato kwenye vipodozi.
• Steroids zikitumika kwa muda mrefu husababisha madhara mbalimbali kaam, ugonjwa wa ngozi na kutokwa na chunusi kubwa. Pia ngozi huwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji kidonda hakitapona. Pia husababisha magonjwa ya moyo.

10. CHLOROFORM
• Husababisha kansa ya utumbo mpana na kibofu cha mkojo
• Husababisha ugonjwa wa akili na ugonjwa wa mishipa ya fahamu
• Kwenye ngozi, chloroform husababisha ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu sana na kutokwa na vipele.

11. CHLOROFLUOROCARBON (HALOGENATED CHLOROFLUOROALKANES)
• Husababisha madhara kwenye mishipa ya katikati ya fahamu na hivyo kusababisha mtu kutopumua vizuri
• Husababisha kichefuchefu, kutapika, kuumwa na kichwa, kusikia usingizi na kusikia kizunguzungu.

12. METHYLENE CHLORIDE
• Husababisha satarani/kansa (cancer)
• Husababisha madhara kwenye mishipa ya kati ya fahamu, kwenye maini na kwenye mishipa ya moyo.
Pamoja na madhara ya kiafya yaliyotajwa hapo juu pia kuna madhara mengine ya kiuchumi yanayoweza kuambatana na matumizi ya vipodozi visivyo na ubora na usalama kwa mtumiaji.
• Kwanza ni gharama za matibabu pale mtu anapopata madhara
• Lishe kwa watoto na familia kwa ujumla hupungua kwa sababu pesa nyingi hutumiak kununua vipodozi au mikorogo.
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), inapenda kuwaasa watumiaji wa vipodozi na wananchi kwa ujumla kujiepusha na matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kwani huleta madhara ya afya kwa mtumiaji.

STARZTZ

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974