Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
26 Apr

CLINTON NA TRUMP WAPIGANIA MAJIMBO YA MASHARIKI.

Published by elipidius geofrey  - Categories:  #HABARI

CLINTON NA TRUMP WAPIGANIA MAJIMBO YA MASHARIKI.

Wapiga kura katika majimbo matano kaskazini mashariki mwa Marekani watapiga kura katika uchaguzi wa mchujo wa kuteua wagombea wa vyama vya Republican na Democratic.

Majimbo hayo ni Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania na Rhode Island.

Matokeo ya uchaguzi huo huenda yakaimarisha uongozi wa Hillary Clinton wa Democratic na Donald Trump wa Republican.

Bi Clinton na Bw Trump wanaongoza kwa kiwango kikubwa katika majimbo yote matano kwa mujibu wa kura za maoni za karibuni zaidi.

Wapinzani wa Bw Trump tayari wanaonekana kukubali kushindwa na hawaangazii majimbo hayo.

Ted Cruz na John Kasich badala yake wanasaidia kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura majimbo ya Indiana, Oregon na New Mexico.

Bw Trump ameshutumu mpango wao akisema ni ishara ya udhaifu na kutamauka.

Trump ayumbayumba kuhusu utoaji mimba
Clinton na Sanders wajibizana kuhusu Obama

Wiki iliyopita, Clinton na Trump, walipata ushindi mkubwa katika jimbo muhimu la New York.

Wadadisi wa mambo wanasema huenda Bi Clinton akawa amejihakikishia ushindi wa tiketi ya chama cha Republican kufikia Jumatano.

Bw Trump bado ana safari ndefu lakini ushindi kwenye majimbo hayo matano utamfanya kukaribia idadi ya wajumbe 1,237 inayohitajika kuifanya vigumu kwake kupokonywa tiketi ya chama hicho.

STARZTZ

Comment on this post

About this blog

Kwa matangazo mbalinbali wasiliana nami kupitia, 0714260485,0759110974